Slide
Ukinichangia, umenisaidia niishi. Kupandikizwa Figo ni gharama. Dialisis inaumiza, Mara 3 kila wiki

Kwa kifupi, kuchangia fedha ya kupandikiza figo ni kuchangia maisha mapya na matumaini mapya.
Ndugu yangu, ninaomba unichangie. Nimepata msamalia mwema wa kunipa figo. Asante kwa kuchangia maisha yangu.

previous arrow
next arrow
Shadow

Karibu tumsaidie

Wimbo wa Ibada

Mimi ni Gadi Sedekia. Hali yangu ya afya siyo nzuri, kwa sababu sipati haja ndogo. Figo zangu zote hazifanyi kazi. Kwa msaada wa mashine maalum za kuondoa sumu mwilini ninaishi, ila kwa maumivu makali sana.

Naomba Unichangie Fedha Sasa

Sadaka yako nitumie moja kwa moja kwenye akaunti zangu(Gadi Sedekia) kama ifuatavyo:

Benki ya NMB: 42510005391

M-PESA: +255 765 113 586

Jina: GADI KAPARARE SEDEKIA

Natanguliza SHUKURANI,

Mwenyezi Mungu Akubariki Sana.

Nisikilize nikihojiwa na “Simulizi na Sauti”

Sukari ilianza kunisumbua nikiwa na miaka 19. Kisha likafuata shikizo la damu, na sasa imepelekea figo kushindwa kufanya kazi. Nilipambana na kumudu kuishi kwa uzoefu na kuwasaidia wengine waliokata tamaa hasa waliosumbuliwa na ugonjwa wa Sukari.

January 1, 2009

Sukari (Diabetic)

Nilianza kuwa na dalili za kudhoofika afya. Nilipopima nikagundulika nina Kisukari.

January 1, 2009
January 1, 2023

Shinikizo la Damu (Pressure)

Baada ya changamoto nyingi, nilihisi kuchoka zaidi ya vile nilivyozoea. Nilipima Hospitalini nikagundulika nina shinikizo la Damu, yaani Presha

January 1, 2023
January 1, 2023

Nilianza kutumia dawa

Daktari alipoona hali yangu inazidi kuwa mbaya alinianzishia dawa na kupewa ushauri wa kitabibu ili kupambana na magonjwa mawili, Sukari na Presha.

January 1, 2023
January 1, 2024

Nilianza Dialysis

Hali ilizidi kuwa mbaya, miguu ikavimba sana, kumbe figo zinaleta shida. Nikaanza kufanyiwa Dialysis. Mount Meru Hospital, Arusha.

January 1, 2024
January 1, 2024

Maisha ya Dialysisi yakaendelea

Nikafanyiwa upasuaji mdogo wa kupandikiza king’amuzi cha kusaidia kufanya Dialysis.

January 1, 2024
January 1, 2025

Maisha ya Dialysisi yakaendelea

Maendeleo yangu yakazidi kuwa mabaya hadi kufanya Dialysis Mara TATU kwa wiki

January 1, 2025
January 1, 2026

Mpango wa kupandikizwa Figo

Niliwasiliana na Familia na kuamua kutafuta msamalia wa kunisaidia Figo, wakapatikana, na sasa nahitaji Mchango ili nifanikishe matibabu

January 1, 2026

Ugonjwa ulianza nikiwa kidato Cha Sita nikikaribia kumaliza. Niliendelea na maisha ya shule nikiwa na Sukari. Na sasa napambana na Dialysis. Naomba mchango wako ili kupandikiza Figo.

Kupandikizwa figo ni tiba bora kuliko dialysis ya muda mrefu, lakini inahitaji ufuatiliaji wa karibu na matumizi ya dawa za kudhibiti kinga maisha yote.

Mtu hupandikizwa figo pale figo zake zimeharibika kabisa na haziwezi tena kufanya kazi ya kuchuja damu, kutoa sumu mwilini, na kudhibiti maji na chumvi. Hii mara nyingi hutokana na ugonjwa sugu wa figo (chronic kidney disease) au figo kushindwa kabisa kufanya kazi (end-stage renal disease).

Kushindwa kwa Figo (End-Stage Renal Disease)

Figo zikishindwa kufanya kazi kwa zaidi ya 85โ€“90%, mgonjwa anahitaji dialysis au kupandikizwa figo.
Dialysis huchuja damu kwa mashine, lakini transplant hutoa suluhisho la kudumu zaidi.
Matatizo ya Kizazi au Majeraha

Magonjwa Yanayosababisha Uharibifu wa Figo

Shinikizo la damu sugu (Hypertension) โ€“ linaweza kuharibu mishipa ya damu ya figo.
Kisukari (Diabetes mellitus) โ€“ husababisha nephropathy, moja ya sababu kubwa ya kushindwa kwa figo duniani.
Glomerulonephritis โ€“ kuvimba kwa vitengo vya kuchuja damu ndani ya figo.
Polycystic kidney disease โ€“ ugonjwa wa kurithi unaosababisha uvimbe (cysts) kwenye figo.

Gadi ni kijana mdogo

Gadi ni kijana mdogo, ana umri mdogo na bado ana ndoto nyingi sana. Kwa sasa ana matumaini makubwa ya kutimiza ndoto zake hasa zinazohusiana na kusaidia jamii. Anahisi kuwa bado kuna mambo makubwa au ndoto kubwa ya mambo ya kutimiza katika jamii na dunia kwa ujumla. Hebu tuangalie kidogo kazi zake za mziki wa injili na huduma za jamii ambazo ni sehemu ya ndoto zake;

Kupandikiza figo hutoa faida kubwa kiafya kwa wagonjwa wenye kushindwa kwa figo, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa muda wa kuishi, ubora wa maisha, na uhuru kutoka kwa mashine za dialysis. Ni tiba bora zaidi kuliko dialysis kwa wagonjwa wengi wa ugonjwa wa figo wa hatua ya mwisho.

Faida za Kupandikizwa Figo ni hizi hapa;

Kuboresha ubora wa maisha

Close-up view of hemodialysis equipment for kidney failure in intensive care unit
Ataweza kuishi bila kutegemea dialysis mara kwa mara.
Atapunguza vikwazo vya ratiba kali za dialysis ( mara 3 kwa wiki kwa saa kadhaa).
Figo iliyopandikizwa itafanya kazi karibu sawa na figo ya kawaida, kusaidia mwili kuondoa sumu na maji.

Afya bora ya muda mrefu

Atapunguza hatari ya matatizo ya moyo na mishipa yanayohusiana na dialysis.
Atapata nguvu zaidi, atalala vizuri, na ataweza kushiriki kikamilifu katika shughuli za kila siku.

Uhuru zaidi

Atanaweza kusafiri na kufanya shughuli za kawaida bila vizuizi vingi.
Hatahitaji tena dialysis, ambayo ni mchakato wa kuchosha na unaoweza kuwa na madhara ya muda mrefu.

Mchango wako wa matibabu ni muhimu kwa sababu gharama za matibabu ni kubwa na siwezi kuzifikia kwa urahisi peke yangu.

Hapa kuna sababu kuu kwa nini mchango wako wa matibabu ni wa maana sana kwangu:

 Kuokoa maisha:

Upandikizaji wa figo mara nyingi ni suluhisho pekee kwa wagonjwa wenye figo kushindwa kufanya kazi. Bila msaada huu, wagonjwa wengi hutegemea dialysis maisha yote, ambayo ni ngumu na yenye gharama kubwa. 

Kupunguza mateso:

Dialysis inachosha mwili na akili. Figo jipya linaweza kumruhusu mgonjwa kuishi maisha yenye afya na uhuru zaidi. 

Gharama kubwa: 

 Upandikizaji wa figo ni mchakato wa kitabibu unaohitaji vifaa, madaktari bingwa, dawa za kupunguza kinga, na ufuatiliaji wa muda mrefu. Michango husaidia kufidia gharama hizi ambazo mara nyingi mgonjwa peke yake hawezi kumudu.  

Ni Mtu akipata figo jipya na kupona, anaweza kurudi kazini, kusaidia familia yake, na kuchangia maendeleo ya jamii.  

Ubinadamu na mshikamano:

Kuchangia ni tendo la huruma na mshikamano wa kijamii. Ni njia ya kuonyesha upendo na mshikamanio kwa wale wanaopitia changamoto kubwa kiafya.  s

Maisha Mapya na Matumaini Mapya.  

Kwa kifupi, kuchangia fedha ya kupandikiza figo ni kuchangia maisha mapya na matumaini mapya.  

 Kupunguza mzigo wa kifamilia:

Familia hupata nafuu kwa sababu mgonjwa anakuwa na afya bora na si tegemezi sana.  

Pia atapona, na kurudi kazini, kusaidia familia yake, na kuchangia maendeleo ya jamii.  

Mwenyezi Mungu Akubariki kwa maana sadaka yako ni kama ifuatavyo:

Ni ishara ya upendo kwa Mungu na kwa watu.
Ni mbegu ya baraka โ€“ Biblia inasema anayepanda kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu (2 Wakorintho 9:6).
ย Ni ushirikiano na kazi ya Mungu โ€“ Tunapotoa, tunashiriki katika kuendeleza injili na kusaidia wahitaji.ย 

Kanuni za Utoaji wa Kibiblia zinatutaka tutoe namna hii;

Toa kwa moyo wa furaha โ€“ Utoaji si mzigo bali ni ibada ya shukrani.
Toa kwa imani โ€“ Tunatoa tukiamini Mungu ndiye chanzo cha riziki.
Toa kwa ukarimu โ€“ Kusaidia wahitaji, maskini, wajane, na yatima (Yakobo 1:27).
Toa kwa heshima kwa Mungu โ€“ Sadaka na zaka ni upendo wa kumheshimu Mungu kwa mali zetu
Toa kwa uwajibikaji โ€“ Uwe utoaji wa kweli na si wa unafiki (Matendo 5:1-11, Anania na Safira).ย ย